Breaking News

Nilipokuwa Bado mdogo,mwenye miaka sita au saba tu,siku moja nilifanya kosa Kubwa.sikumbuki ni kosa gani

Nilipokuwa Bado mdogo,mwenye miaka sita au saba tu,siku moja nilifanya kosa Kubwa.sikumbuki ni kosa gani,lakini najua lilikuwa kubwa kwasababu Baba yangu alinipiga.Alikuwa anipigi mara nyingi,lakini siku hiyo alinichapa vibaya akiwa amekasirika sana.Ndipo alisema ‘’Nenda chumbani ukafungishe nguo zako na uondoke Hapa nyumbani.’’Basi nilikwenda Chumbani,nasi tulikuwa maskini,Nilikuwa na Nguo chache tu,Nilizitia katika mfuko mdogo,Nikaenda Mlangoni,Na Baba alinipa shilingi moja tu akaniambia,’’Nenda ukachukue Bus mpaka Nyumba ya watoto Yatima.’’akasema,’’Umekuwa Mtundu paka mama yako na Baba yako hatukutaki tena.’’

Basi nikiwa na mfuko katika mkono mmoja,na shilingi moja katika mmkono mwingine,Nilitoka  mlangoni na kutembea karibu na kituo Cha Bus,ndipo mama angu alinifuata akikimbia,akaniambia’’Rudi,rudi,hatukumaanisha Hivyo.”Basi niligeuka nikarudi Nyumbani na Mama.lakini Ndani Yangu nikilia sana,kulikuwa na maumivu makali sana moyoni mwangu.Ikiwa wewe ni mama au Baba utafahamu vema maumivu ya moyo wa mtoto.Tatizo ya maumivu hayo ni kwamba niliendelea kukua nikiamini kwamba watu walioniambia kwamba wamenipenda,Siku moja wangenikatalia.

Na ukiwa unatazamia kukataliwa ,utajisikia umekataliwa na watu wote kila mara,Ingawa sivyo Ilivyo.

Watu wengi wamekuwa na maumivu ya ndani Bila kupata msaada,wengine wamekataliwa na wenzi wao,wazazi ,ndugu  na  Jamii kadhalika wengine wameonewa na kuteswa na kunyimwa Haki zao za msingi.Watu Hawa wanahitaji uponyaji wa ndani wa mioyo yao,Inatupasa kufikiri  kwamakini maana ya maumivu .

kuna mambo Muhimu ya kueleza ;kwanza,Tutawatambuaje watu wenye maumivu Hayo??Pili,Uponyaji wa ndani ni nini??
Njia Bora ya kujifunza juu ya uponyaji wa ndani ni njia ya Matendo,na ndivyo tunavyofanya baada ya maelezo katika Semina zetu za Hapa na pale.Ikiwa Inaonekana kwamba ni kughafilisha,naweza kujibu kwamba Ndivyo Bwana Yesu alivyofanya.aliwaambia wale Theneshara’’Wapeni ninyi Chakula’’-watu elfu tano!!wala hakuwaambia wawalishe kwa njia gani,alisema tu’’Wapeni Chakula’’walipomtii hatua kwa Hatua,muujiza Ulitotokea.naabaadaye walikaa Chini kuulizana ‘’Hilo liliwezekanaje??’’

Basi Uponyaji wa maumivu ya ndani Nini?
Kuna maumivu ambayo yanaendelea kuumiza  na kutujengea makumbuko Mabaya,hali ya Hofu ya kushindwa kuhusiana kama kawaida na wanaume(kama ni mwanamke)au wanawake(kama ni mwanaume);Hali hii inamfanya mtu ajizuie  asimpende mtu mwingine kusudi asiumizwe Tena.na Matokeo ya namna hii katika maisha ya kila siku ni Ugonjwa au Dhambi;yaani Hali ya kukata tama,kujisikia kuwa haufai,Hofu zisizo na sababu,Magojwa yanayosababishwa na mawazo,Hadi hamu ya kujiiua  pia inatokea wakati mwingine.Ndyo maana tunahitaji UponyaJI Wa Ndani.

Hizo ndizo Namna ya maumivu ya Ndani ambazo Mungu anataka kuzigusa na mkono wake wa uponyaji.sasa  utatambuaje asili ya shida ya Yule mtu anayekujia na kusema kwamba ana maumivu ya ndani?utagunduaje kiini cha shida ile?Inatupasa tuzungumze na kuhojiana naye polepole kuhusu mambo ya kimwili,kiakili na kiroho pia.unapoelezana na mtu Yule unajiuliza ‘’mtu Huyu ni wa aina gani?Ni muhimu kufanya hivyo.

Bwana Yesu alijua kwamba Nathaniel alikuwa tofauti na petro na Andrea na mariamu.aliweza kumwelewa kila mmoja kwasababu aliwafahamu mmoja mmoja.wakati mwingine ni muhimu zaidi kuwafahamu kwamba Huyu mwenye maumivu ni mtu wa aina gani,kuliko kuelewa ni aina gani ya mauimivu aliyonayo.
maana watoto wawili waliotokana na nyumba mbili zenye shida ileile ya kuachana na wazazi wao,wataitikia njia ile kwa njia Mbili Tofauti.

Basi inakupasa ujifunze yote uwezayo juu ya wakati ukujiao.Usiogope kujifunza mambo ya watu na kuwafahajhmu na kupata ujuzi wa kukaa na watu wa kila aina.Mungu atatumia uzoefu huo akikuwezesha kuwafahamu kwa Ndani.
     
           Usikose ku download application yete BOFYA HAPA https://play.google.com/store/apps/details?id=com.masangula

No comments