Breaking News

Mwanafunzi wa darasa la sita Shule y a Msingi  abakwa mpaka kufa

Mwanafunzi wa darasa la sita Shule y a Msingi Kapanga Kata ya Katuma Tarafa ya Mwese Wilaya ya Tanganyika Veronica Lucas 13 amekutwa akiwa amekufa baada ya kubakwa hadi kufa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupiwa kwenye shimo la kolongo.Mwandishi wa Malunde1 blog,Walter Mguluchuma.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benedict Mapujila alisema tukio hilo la mauaji ya kinyama lilitokea juzi majira ya saa kumi na moja na nusu jioni Kijijini hapo .

Alisema siku hiyo ya tukio Veronica aliondoka nyumbani kwao kama ambavyo huwa kawaida yake kwenda shule kwa ajili ya masomo katika shule ya msingi aliyokuwa akisoma ya Kapanga .

Alieleza kuwa marehemu baada ya kuwa amekwenda shuleni hakurudi tena nyumbani kwao hali ambayo iliwafanya wazazi wake wapate shaka kwani hakuwa na tabia ya kutorudi nyumbani kwao.

Siku iliyofuata wazazi wake na marehemu walikwenda kufuatilia shuleni na hawakuweza kumkuta hali ambayo ilizidi kuwatia wasiwasi zaidi na waliamua kwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho .

Viongozi wa kijiji pamoja na wananchi wa kijiji hicho waliamua kuanza kumtafuta kwenye maeneo mbalimbali ya kijiji hicho kwa muda wa kutwa nzima pasipo kukata tamaa.

Kaimu Kamanda alisema ilipofika saa kumi na moja na nusu ya jioni waliukuta mwili wa marehemu Veronica ukiwa umetupwa kwenye shimo la kolongo huku marehemu akiwa amekufa baada ya kubakwa na watu wasiojulkana na sehemu zake za siri zikiwa zimeharibika vibaya.

Alisema chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo wa kike kilitokana na kubakwa na kisha kuvuja damu nyingi na kusababisha kifo hicho cha kinyama na cha kikatili na chakusikitisha .

Alisema  mpaka sasa hakuna mtu wala watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo na jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo la kinyama .

Mwili wa marehemu  baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari walikabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya mazishi ambayo yalifanyika kijijini hapo siku iliyofuata.


No comments