Movie kati ya Ronaldo na Manchester United yaanza upyaaa.....
Hakuna ajuae hili movie litaisha lini kwani kila msimu wa usajili linaibuka, baada ya Ronaldo kusema hataki tena kuendelea kucheza soka nchini Hispania, klabu ya Manchester United wameibuka upyaa na inasemekana wanataka kumrudisha Old Trafford.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimesema Manchester United wanataka kujaribu kutuma ofa kwa Real Madrid kuona kama wanaweza kukubali kumuuza mwanasoka bora huyo wa dunia mwenye umri wa miaka 31.
Pamoja na vilabu kama PSG na baadhi ya timu kutoka Marekani na China kumtaka mchezaji huyo lakini hakika Ronaldo atapenda kuona ofa ya Manchester United mezani kwa Real Madrid kwa kuwa hapo ndio anapopapenda.
Lakini gazeti la Marca linasema kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane hayuko tayari kumuona Ronaldo anaondoka Real Madrid na tayari ameshaanza kufanya mpango wa kuongea naye kuhusu kubaki Santiago Bernabeu.
Usajili wa Ronaldo kwenda Real Madrid bado unaweza kuwa na vikwazo vingi kwani Real Madrid toka dirisha hili la usajili lianze wanaonekana kuwawekea vikwazo United katika suala la kununua wachezaji wao.
Kama unakumbuka Unitec wameshajaribu kumnunua Bale ikashindikana na sasa wamewekewa kiwingu katika usajili wa Alvaro Morata na James Rodriguez ambao wote wanawataka.
No comments