Kocha Nakuru: Tunataka ushindi dhidi ya Gor Mahia
KOCHA Msaidizi wa timu ya Nakuru All Stars Jimmy Angila amesema kuwa mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Sportpesa Super Cup 2017 dhidi ya Gor Mahia utakuwa ni mgumu sana ila wana imani watatoka na ushindi.
Akizungumza na mtandao huu, Angila amesema kuwa katika mchezo wao huo hawatakubali kuona wanapoteza kwani kwa wao ni muhimu sana kuingia fainali na cha zaidi hawataingia kwa kuidharau bali watahakikisha wanashinda.
Amesema kuwa, wanaifahamu vizuri timu ya Gor Mahia na zaidi wanatarajia mechi hiyo kuwa ngumu sana kwa kila upande.
"mechi yetu dhidi ya Gor Mahia ni ngumu sana ila tutaingia uwanjani kwa kuhakikisha tunashinda mchezo huo ambao ni muhimu sana kwetu kwani lengo letu ni kuingia fainali,"amesema Angila.
Angila alisisitiza kuwa kikosi chao kipo vizuri na benchi la ufundi ndiyo litapanga kikosi cha kesho na mabadiliko yanaweza kufanywa kulingana na hali za wachezaji.
Daktari wa timu ya Nakuru Vicent Angwenyi amethibitisha kutokuw ana majeruhi katika kikosi chao na zaidi wote wanaweza kucheza katika game mechi ya kesho dhidi ya Gor Mahia.
Timu hizo kutoka Kenya zinakutana katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Sportpesa Super Cup 2017 na mchezo huo unatarajiwa wa ushindani mkubwa kwani timu hizo mbili zinajuana huku Gor Mahia ikiwa inashiriki ligi kuu ya Kenya na Nakuru ikiwa ligio darala la kwanza.
No comments