Breaking News

Kamanda Mpinga kuhusu walichogundua ukaguzi mabasi ya wanafunzi


Story ya baada ya tukio la ajali iliyoua watu 35 wakiwemo wanafunzi 32 Arusha, ilikuwa ni kuhusu kufanyika kwa ukaguzi wa magari ya wanafunzi yaani School Buskuangalia ubora wake na kama yanafaa kubeba wanafunzi.

Ayo TV na millardayo.com zimemtafuta Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa PolisiMohammed Mpinga ambaye anaelezea zaidi akianza kwa ufafanuzi wa zoezi hilo akisema ingawa lilianza kabla ya ajali lakini sasa kikosi hicho kimeongeza nguvu zaidi.

“Zoezi la ukaguzi wa mabasi ambayo yanachukua wanafunzi mashuleni kwa maana ya kuwapeleka shuleni na kuwarudisha nyumbani, ni zoezi ambalo tumelianza kwa nguvu kubwa na hasa likichagizwa na ajali ambayo ilitokea kule Karatu mkoani Arusha. Niseme tu kwamba, sio kwamba tulianza kwa sababu ya ile ajali lakini tulikuwa tukifanya huko nyuma lakini baada ya tukio lile tumeanza kulifanya kwa nguvu kubwa zaidi.” – Kamanda Mpinga.

Aidha, Kamanda Mpinga amesema kuwa ukaguzi huu umefanywa nchi nzima ambapo wamekuwa wakikagua uzima wa magari, sifa za madereva wanaoendesha mabasi ya wanafunzi, kufuatwa taratibu za SUMATRA.

No comments