FAHAMU KWA NINI MAGARI YA SERIKALI HAYANA BIMA WALA KADI YA GARI*
FAHAMU KWA NINI MAGARI YA SERIKALI HAYANA BIMA WALA KADI YA GARI*
*Tujikumbushe sheria!!!*
*KWA NINI MAGARI YA SERIKALI HAYANA BIMA WALA KADI YA GARI*
Ni kweli kwamba magari ya serikali yakiwemo ya polisi huwa hayana stika za bima wala madereva wake kutembea na kadi ya gari.
Utaratibu wa usajiri wa magari ya Serikali ni tofauti kidogo na utaratibu unaotumika kwenye magari mengine yasiyo ya serikali.
Magari ya serikali kwa sasa hayasajiliwa mamlaka ya mapato (TRA) ingawa utaratibu unafanyika ili nayo yasajiliwe TRA.
Kwa sasa magari yote ya serikali yanasajiriwa kwa utaratibu wa wizara ya ujenzi na yanakuwa na kadi inayoitwa *“Certificate of Motor vehicle, motor cycle, tricycle and plant Registration”* kutegemeana na aina ya chombo husika. Magari hayo hayakatiwi bima bali kwa jambo lolote linalotokea ambalo kwa magari ya kawaida yangehitaji huduma za bima kwa magari hayo malipo yote au madai/malalamiko hupelekwa wizara ya Fedha kwenye ofisi ya msimamizi wa mali za serikali ambae hutoa fidia kwa kuwasiliana na wizara ya Ujenzi.
Ikitokea gari la serikali limepata ajali au kusababisha uhalibifu kwa chombo au mali ya mtu mwingine lazima taarifa zake zifikishwe katika wizara hiyo ili ishughurikie taratibu za matengenezo ya magari hayo pamoja na magari ya kiraia ambayo yamesababishiwa ajali na magari hayo ya polisi au ya serikali kwa ujumla.
Lakini inashauriwa taarifa hizo zitolewe Kama ajali hiyo imesababisha majeruhi na kwamba thamani ya uharibifu wake unazidi shilingi laki tatu (300,000/=) chini ya hapo mhusika aliyesababisha ajali anaweza kumaliza mwenyewe au kupitia idara yake.
Taarifa hiyo hutolewa kwenye fomu namba T.F.N 80 kwenda kwa mkuu wa idara ambayo gari lake limesababisha ajali au limepata ajali.
Kama itaonekana kuwa kuna madai serikali inabidi walipe au kuna gharama za kutengeneza gari hilo la serikali basi itapasa polisi kikosi cha usalama barabarani wanao shughurikia ajali hiyo watume nakala nne za PF.90 pamoja na T.F.N 80.
Tukumbuke kwamba wakati kwa magari ya kiraia makadirio ya gharama hufanywa na garage za kawaida na kujaza kwenye _profoma invoice_ kwa upande wa magari ya serikali
Makadirio ya gharama yanafanywa na garage za serikali chini ya wizara ya ujenzi (TEMESA) hivyo hata kama gari la kiraia limesababishiwa ajali na kutakiwa kulipwa na serikali basi madai yake lazima yasibitishwe na TEMESA.
Nimalizie kwa kusema kuwa *"madereva wa serikali hawako juu ya sheria na wanatakiwa wakati wote kutii sheria za usalama barabarani na watashitakiwa kama madereva wengine wa kiraia pindi wakisababisha ajali au kosa lolote la usalama barabarani"*
Tofauti ipo kwenye utaratibu tu wa chombo cha kulipa fidia, vyombo ambavyo siyo vya serikali fidia hulipwa kupitia makampuni ya bima ambako mhusika alikatia bima lakini kwa magari ya serikali fidia hulipwa kutoka wizara ya fedha kupitia wizara ya ujenzi ambao ndio wenye dhamana ya magari yote ya serikali.
No comments