Breaking News

Asiyeona, wala kusikia ahukumiwa kunyongwa

MAMLAKA za Saudi Arabia zimepanga kuendelea na mpango wa kumnyonga mwanamume mwenye ulemavu wa usikivu na macho kwa shtaka la kushiriki maandamano.

Mtu huyo, Munir Adam (23), alikamatwa wakati wa maandamano ya kisiasa katika mji unaokaliwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia, mashariki mwa ufalme huu mwaka 2012.

Mahakama ya Saudi Arabia iliridhia adhabu ya kifo iliyopitishwa awali na Adam sasa amebakiwa na rufaa moja kabla ya Mfalme kusaini hati ya kumnyonga.

Uamuzi huo wa mahakama unakuja huku wanaharakati wakimlalamikia Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kushindwa kuzungumzia suala la ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa ziara yake katika ufalme huo.

Kwa mujibu wa Reprieve, Adam ambaye alipata ulemavu huo wa usikivu na kuona wakati alipopata ajali akiwa mtoto mdogo, alikamatwa kwa kile kilichoelezwa vurugu na kutuma ujumbe wa uchochezi.

Lakini wanaharakati wanadai kwamba ‘kauli ya kulazimishwa’ ilitumika kama ushahidi pekee kumtia hatiani katika kesi iliyoendeshwa kwa siri.

No comments