Shilole, Nay wa Mitego na Kala Jeremiah waongea kuhusu picha za Ben Pol
May 22, 2017
Moja ya picha zilizopata comments nyingiInstagram siku mbili hizi ni picha za mwimbaji wa RNB Tanzania Ben Pol ambazo zilimuonyesha akiwa hajavaa nguo.
Ben Pol hajaongea chochote mpaka sasa kuhusu picha hizo lakini walioongea wengi ni mashabiki na baadhi ya Mastaa wenzake wakisema wamezichukuliaje picha hizo.
NAY WA MITEGO: ‘Sijui amelenga nini… sitaki kuhukumu ile picha, bwana Benard mimi sitaki kuzungumzia hii picha yako, ngoja tusikie neno kutoka kwake sababu mimi sijasikia akizungumzia chochote, nimemtumia msg hajanijibu‘
SHILOLE: ‘Siwezi kujua alifikiria nini kuipiga ile picha ila nilipoiona ile picha nilishtuka kidogo sababu namjua Ben Pol na yale mambo huwaga ni tofauti, yale mambo huwa tunafanya sisi watoto wa kike’
KALA JEREMIAH: ‘Mimi najua account ya Ben Pol imekuwa hacked, nilivyoona picha niliamini watu ndio wameedit zile picha siamini kama ni Ben Pol, ni mtu namuheshimu sana‘
Hayo ni machache tu kati ya waliyoyasema Nay wa Mitego, Shilole na Kala Jaremiah…
No comments