PICHA 15: Jay Z na Beyonce walivyovalia Kiafrika kwenye curter push party
May 22, 2017
Mastaa wa dunia Jay Z (47 yrs) na mke wakeBeyonce (35) wameichukua trend tena baada ya kutokelezea kwenye picha za pamoja wakiwa wamevalia kiafrika.
Beyonce ambaye anatarajia watoto mapacha aliwaalika watu mbalimbali kwenye ‘baby shower‘ waliyoipa jina la ‘Curter Push Party‘ iliyohudhuriwa pia na watu mbalimbali maarufu wakiwemo Serena Williams, Tina Knowles ( Mama Beyonce), La La Anthony, Vanessa Bayer na Kelly Rowland.
Ni party ambayo watu walivalia kiafrika zaidi na hata burudani zilizokua zikitolewa ngoma ilihusishwa huku Jay Z pamoja na kuvalia lakini pia ‘alitundika’ ramani ya Afrika kifuani.
Mwimbaji Kelly Rowland akionekana kumuwekea Beyonce nguo yake sawa
Kelly na Michelle wakiwasili kwenye party
No comments