RAIS MAGUFULI AONYESHA NIA YA DHATI AFANYA MAPINDUZI YA ELIMU
Rais Magufuli afanya mapinduzi ya elimu
Rais Magufuli ametajwa kuwa rais wa kwanza mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu nchini baada ya kuruhusu serikali yake kutumia zaidi ya shilingi bilioni 18 kila mwezi kugharimia elimu ya msingi na sekondari
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wazazi wa shule sita za msingi katika kata ya Ihyela, Mbeya baada ya kukusanyika kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi 10 wa darasa la saba ambao wamefanya vizuri mtihani maalum wa majaribio wa maandalizi ya mtihani wa taifa unaotarajiwa kufanyika miezi michache ijayo.
Akizungumza kwa niaba ya walimu, Mratibu wa elimu kata ya Ihyela Dickson Sinkwembe, ameahidi kuwa walimu watahakikisha wanafunzi 10 ambao wamefanya vyema mtihani huo wa maandalizi, wanapata matokeo mazuri kwenye mtihani wa taifa na kuiletea heshima kata hiyo, huku akiwataka wazazi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu.
Pamoja na hayo, mdau wa elimu katika kata hiyo, Bw. Ndele Mwanselela amewapatia zawadi wanafunzi hao ya fedha taslimu huku akiwataka wananchi kumuunga mkono Rais JPM kutokana na uamuzi wa serikali yake kutumia zaidi ya Shilingi bilioni 18 kila mwezi kwa ajili ya kugharamia elimu.
No comments