N’Golo Kante ameshinda tuzo nyingine
Michezo
May 19, 2017
Kiungo staa wa Ufaransa anayeichezea Klabu ya Chelsea ya England N’Golo Kante ametwaa tuzo nyingine msimu huu mara hii ikiwa ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Waandishi wa Habari za Michezo, FWA.
Katika hafla iliyofanyika Landmark Hotel Kante alipigiwa kura kushinda tuzo hiyo akiwapiku mchezaji mwenzie wa Chelsea Eden Hazard na mchezaji wa Tottenham Dele Alli kwa zaidi ya 65% ya kura zote.
Kabla ya tuzo ya FWA tayari N’Golo Kante alitwaa tuzo ya PFA na sasa anakuwa mchezaji wa 20 kutwaa tuzo hizo mbili kwa mkupuo mmoja.
Kiungo wa Chelsea N’Golo Kante akiwa na tuzo yake ya FWA
Mwenyekiti wa FWA Patrick Barclay (kushoto) akimkabidhi N’golo Kante tuzo ya FWA
N’golo Kante baada ya kutwaa tuzo ya FWA
No comments