Kocha Serengeti Boys amezungumzia tatizo la umaliziaji
May 19, 2017
Timu ya Serengeti Boys huenda ingepata ushindi wa magoli zaidi ya mawili kama ingetumia vizuri nafasi zilizotengenezwa wakati ikipambana na Angola kwenye mechi ya pili ya Kundi B ya michuano ya AFCON U17.
Kocha msaidizi wa Serengeti Boys Oscar Mirambo amesema, wachezaji wanapaswa kufahamu umuhimu wa nafasi zinazopatikana na kuzitumia.
“Kwa sasa kwa maana ya kufanya mazoezi hakuna kitu ambacho unaweza kufanya kutokana na muda ulivyo, kitu ambacho unaweza kukifanya sasa hivi ni mental training ili watoto waweze kuelewa umuhimu wa nafasi wanazozipata ili waweze kuwa makini kuzitumia.”
“Mechi ya kwanza tulikuwa tuna-defend na hatukuwa na namna iliyokuwa sahihi ya kushambulia kulingana na mpinzani tuliyekutana nae, mechi dhidi ya Angola tulijaribu kushambulia, tuliruhusu watoto washambulie na tunashukuru tukaweza kufunga magoli mawili.”
“Kama tungekuwa na hiyo game plan tangu mechi ya kwanza inawezekana matokeo yangekuwa tofauti tungeweza kutengeneza nafasi nyingi na kupata matokeo.”
Serengeti Boys ilishinda 2-1 dhidi ya Angola na kufikisha pointi 4 sawa na Mali ambao nao walishinda 2-1 dhidi ya Niger. Jumapili Mei 21, 2017, zitachezwa mechi za mwisho za makundi na timu nne (mbili kutoka kila kundi) zitasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.
No comments