Breaking News

Nay Kufanya Shoo ya Bure Karume Leo

MAY 19, 2017

Facebook0Twitter0Google+0WhatsAppViber

STAA wa Ngoma ya Wapo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anatarajiwa kufanya shoo ya bure leo (Mei, 19) katika Viwanja vya Karume jijini Dar ikiwa ni maandalizi ya kuelekea shoo ya kibabe itakayofanyika kesho (Mei 20) katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Showbiz, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, Nay ataambatana na wakali kibao watakaomsindikiza katika shoo hiyo na lengo ni kuwapa mashabiki kile wanachokitaka. “Shoo ya Karume itakuwa bure, naomba umwambie na mwenzako, hakutakuwa na kiingilio chochote!

Shilole.

Nay atafanya shoo na wakali wengine wanaotikisa kama Kala Jeremiah anayetikisa na kibao cha Wana Ndoto, Shilole cha Hatutoi Kiki, Barnaba anayebamba na Malaika pamoja na msanii wa vichekesho, Mkali Wao.

“Tunatarajia shoo ya bure ya Karume kuanza mapema kuanzia saa tano asubuhi ambapo
mbali na Nay kufanya shoo, mashabiki watapata fursa ya kuzungumza naye machache kwa maana ni nadra kwa mashabiki kupata nafasi hizo adimu,” alisema Mbizo.

Naye Nay alitia neno kuwa, mashabiki wajitokeze kwa wingi katika Viwanja vya Karume kwani watatoa shoo ya kishindo. “Nikisema Wapo mnajua namaa-nisha nini? Njooni Karume tuimbe Wapo kwa pamoja. Hakuna kiingilio ni miguu yako tu! Ila Jumamosi (kesho) kiingilio kitakuwa sawa na bure yaani shilingi 5,000 tu,”alisema Nay.

No comments