MICHEZO Kocha wa Dortmund, Thomas Tuchel aachia ngazi
Kocha wa klabu ya Borussia Dortmund, Thomas Tuchel ameamua kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kuiongoza kwa miaka miwili.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43 alichukua mikoba ya kocha Jurgen Klopp’s mwaka 2015 ya kukinoa kikosi hiko.
Kocha wa klabu ya Borussia Dortmund, Thomas Tuchel
Dortmund ilifanikiwa kutwa kombe la Ujerumani DFB Cup siku ya Jumamosi baada ya kuifunga klabu ya Eintracht Frankfurt. Lakini pia klabu hiyo imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ya ligi ya Bundesliga na hivyo kupata fursa ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya msimu ujao.
Hakukuwa na mahusiano mazuri kati ya kocha Tuchel na Mtendaji mkuu wa klabu, Hans-Joachim Watzke, tangu basi la timu hiyo ya Dortmund lilipo pata ajali ya bomu Aprili 11.
Kocha wa klabu ya Borussia Dortmund, Thomas Tuchel
Taarifa aliyoitoa ndani ya klabu ya Dortmund, imesema kuwa kwa vyovyote hapakuwa na makubaliano baina ya watu wawili, haya yamekuja baada ya mazungumzo kati ya Tuchel na Watzke jumanne hii.Tuchel amedai kuwa si yeye wala wachezaji wake walio shauri mchezo wao wa robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya kuchezwa katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Monaco na kutokea milipuko ya mabomu karibu na basi la klabu hiyo saa 24 kabla ya mchezo wao
Kupitia mtandao wake wa Twitter aliouanzisha siku ya Jumanne, Tuchel alisema “Ninawashukuru wote kwa ushirikiano niliopata katika kipindi chote cha miaka miwili nilichokuwepo mahala hapa. Asante kwa mashabiki, timu, wafanyakazi na wale wote walioonyesha mchango wao kwetu.” Alisema Tuchel .
No comments