Hans Poppe: Namtaka Ngoma na Chirwa Simba
Hans Poppe: Namtaka Ngoma na Chirwa Simba
Zacharia Hans Poppe.
Wilbert Molandi, Championi Jumatano, Habari
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema kama ikitokea akitaka kumsajili mchezaji Yanga, basi atamsajili Mzimbabwe, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Mnyarwanda, Haruna Niyonzima pekee.
Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba walichokaa viongozi wa timu hiyo kutathmini kiwango cha kila mchezaji.
Ngoma na Niyonzima ni kati ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao imemalizika kwenye msimu huu, huku ikidaiwa wapo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kuongezewa na Chirwa yeye amebakisha mwaka mmoja.
Mzimbabwe, Donald Ngoma.
Akizungumza na Championi Jumatano, Hans Poppe, alisema wachezaji hao watatu wa kimataifa pekee ndiyo anaovutiwa nao ndani ya Yanga na akiambiwa awasajili anaweza kufanya hivyo.
Hans Poppe alisema, wachezaji wengine waliobaki viwango vyao ni vya kawaida akiwemo mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe aliyechukua tuzo ya ufungaji bora kwenye misimu miwili ya Ligi Kuu Bara 2015/2016 na 2013/2014, akiwa kwenye timu tofauti Simba na Yanga.
Obrey Chirwa.
Aliongeza kuwa, anavutiwa na Ngoma kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira na kuwatoka mabeki na kwenda kufunga mwenyewe tofauti na Tambwe anayengojea kumalizia mipira pekee golini na kufunga mabao.
“Ndani ya Yanga wapo wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kuja kuichezea Simba, lakini kwangu binafsi ikitokea nikaenda kufanya usajili, basi nitasajili wachezaji watatu pekee.
Haruna Niyonzima
“Ambao ni Ngoma, Chirwa na Niyonzima na kikubwa ninavutiwa na aina yao ya uchezaji ndani ya uwanja na kingine ni wachezaji wanaocheza kwa malengo katika timu.
“Wapo wengine wenye uwezo kama Tambwe lakini yeye ametofautiana na Ngoma kwa uwezo wake wa kumiliki mpira na kuwatoka mabeki akitumia nguvu kwenda kufunga mabao, lakini Tambwe yeye anasubiria kutengewa kwenye kufunga
No comments