KALI KULIKO: Kituko kingine cha Mourinho…mkutano sekunde 10?
May 22, 2017
Meneja wa Manchester United Jose Mourinhoambaye anatajwa kuwa na matukio alifanya kituko cha kufungia msimu wa English Premier Leaguebaada ya kufanya mkutano wa baada ya mechi uliodumu kwa sekunde 10 kwa sababu hakuulizwa maswali.
Mourinho alitakiwa kukutana na waandishi wa Habari kufuatia ushindi wa Manchester United wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa mwisho wa msimu wa EPL 2016-2017 uliopigwaOld Trafford.
Mourinho akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ambao haukuwa na watu wengi baada ya mechi ya Manchester United vs Crystal Palace
Baada ya kuingia kwenye mkutano huo ambao pia haukuwa na watu wengi hakuna mtu ambaye aliuliza swali lolote hivyo Mourinho akasema: “Kwa herini” kisha akaondoka.
Awali akifanya interview na Televisheni ya Klabu‘MUTV’ Mourinho alisema: “Msiniulize mambo mengi kwa sababu najua niko kwenye fainali.”
Muongozaji wa mkutano akiwauliza wanahabari kama wana maswali kwa Mourinho
Baada ya kusubiri kwa sekunde sita bila kuulizwa swali, Mourinho akasema ‘kwa heri’ na kutoka chumba cha mikutano sekunde 10 baada ya kuingia
No comments