Breaking News

TAARIFA ZA AWALI:WALIOMPIGA RISASI TUNDU LISSU WALITUMIA GARI AINA YA NOAH NYEUPE

Kamanda wa Polisi Dodoma amesema yeyote mwenye taarifa kuhusu wahusika waliompiga risasi Tundu Lissu waiwasilishe polisi.

Kwa sasa wamepata taarifa kuwa gari iliyoonekana ni gari nyeupe aina ya Nissan.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma amesema polisi wameshaanza kufanya upelelezi kuhusu wahusika na kusema watu waendelee kusubiri taarifa kutoka kwenye jeshi hilo

Amesema hawatapenda kuona mikusanyiko sehemu yoyote ya Dodoma mjini kwa sababu jeshi la polisi bado linafuatilia asili ya tukio lenyewe na mikusanyiko ya watu inaweza kutumika vibaya.

Pia wataendelea kuwafaamisha raia kwenye kila hatua watakayofikia

No comments