Manji afunguka mahakamani kuhusu kuvuliwa udiwani

Manji alivuliwa udiwani wa Mdagala Kuu kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao
Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji anayekabiliwa na kesi ya kuhujumu uchumi amedai mahakamani kuwa hatambui kuvuliwa Udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu kwa sababu hajapewa taarifa wala barua kutoka Manispaa ya Temeke, inayoonyesha kuwa amevuliwa nafasi hiyo.
Manji amesema hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati shauri lake lilipofikikwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutanjwa.
"Nimeona taarifa kutoka katika gazeti la Mwananchi kwamba nimevuliwa udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu, kama hii taarifa ni ya kweli... mimi siitambui kwa sababu nina miezi miwili nipo gerezani na kama wamenivua walipaswa kunipa taarifa," alidai Manji.
Manji ambaye alitinga mahakamani akiwa amevalia shati jeupe na suruali ya jinsi nyeusi tofauti na siku nyingine, alidai kwa mwaka mmoja uliopita alitoa Sh 70milioni kutoka mfuko wake na sio fedha za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi wake, lakini anashangazwa na kitendo cha kuvuliwa udiwani bila kupewa taarifa kwa sababu alichaguliwa na wananchi.
"Mheshimiwa hakimu kesi niliyonayo ni nzito na DPP hapaswi kuangalia upande wake wa kesi tu, kwani anapaswa kuangalia na upande wangu kwa sababu mimi nimechaguliwa na wananchi," alisema.
"Mheshimiwa hakimu, vikao vya awali vya udiwani wa Halmashauri ya Temeke nilikuwa naudhuria kwa kuwa naheshimu mahakama na kwa uzito wa hii kesi sikutaka kupeleka hata maombi ya dhamana mahakamani," alisema Manji.
No comments