Breaking News

Putin kuapaishwa kwa muhula wa nne kama rais wa Urusi

Vladimir Putin anatarajiwa kuapishwa kwa muhula wa nne kama rais wa Urusi leo Jumatatu baada ya kushinda uchaguzi mnamo Machi.

Amekuwa madarakani kwa miaka 18 kama rais na hata waziri mkuu, na wapinzani wameufananisha muda wake wa uongozi kama utawala wa mfalme.

Polisi wa kupambana na fujo walikabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wake mjini Moscow na katika miji mingine Jumamosi, Kumekuwa na hofu kwamba huenda kutazuka ghasia tena leo Jumatau wakati anapoapishwa.

Sherehe hiyo ya kuapishwa kwake itafanyika Kremlin mjini Moscow na huedna ikawa na ya watu wa karibu tu ikilinganishwa na ile ya mwaka 2012, shirika la habari la AFP Linaripoti.

Putin anatarajiwa kukutana na watu waliojitolea kushughulika wakati wa kampeni yake peke, shirika hilo la habari linasema.

Rais wa kwanza aliyechaguliwa mnamo mwaka 2000, Putin aliwania tena muhula mwingine mnamo mwaka 2004 kabla ya kujiuzulu 2008 ili kuhudumu kama waziri mkuu chini ya mshirika wake Dmitry Medvedev, kwa sababu kisheria, anaruhusiwa kuhudumu kwa mihula miwili pekee mtawalia.

Ilikuwa wazi ni nani aliye na udhibiti na mwaka 2012 Putin alirudi kama rais, kwa mara hii kwa muhula wa miaka sita.

Iwapo na atakapofika mwisho wa muhula wake wa nne mwaka 2024, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 atakuwa amehudumu kwa takriban robo karne madarakani.

No comments