Meli ya kuzalisha umeme yawasili nchini Sudani
Meli hiyo yenye uwezo wa kuzalisha megewatts 180 za umeme inatarajiwa kutoa huduma ya umeme baada ya kusainiwa mkataba na shirika la kuzalisha nishati ya umeme Sudani STPG.
Meli hiyo imewasili katika bandari ya kimataifa ya Sudani na tayari kwa kuanza kutoka huduma ya umeme.
Shirika la "Karpowership" ambalo lina miliki "Karadeniz Powership Rauf Bey" limefahamisha Jumanne kuwa meli hiyo imeanza kutoa huduma ya umeme tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Meli hiyo ni miongoni mwa meli 6 za Uturuki ambazo zinztoa huduma ya umeme barani Afrika. Shirika hilo la uzalishaji wa umeme kutoka nchini Uturuki lina meli zake ambazo zinatoa huduma ya umeme nchini Ghana, Msumbiji, Zambia, Gambia na Sierra Leone.
No comments