Gigy Money Aomba Radhi Baada Ya Kumchana X Wake Hadharan
Mwanamuziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameomba radhi baada ya ugomvi wake na Baba mtoto wake Mo J.
Gigy
Money alimtolea maneno makali Ex wake ikiwemo kuweka wazi kwenye
Interview aliyofanya na Millard Ayo kuwa mtoto wake Myra sio wa Mo J
kwani alikuwa na mwanaume mwingine.
Gigy
Money na Ex wake Mo J walirushiana maneno makali baada ya Gigy
kumtuhumu kuwa hakuwa akimtunza kipindi cha ujauzito na kudai alihama na
kila kitu baada ya kuachana.
Baada
ya sakata hilo Mo J aliongea na vyombo vya habari na kudai kuwa ana
uhakika kuwa mtoto wao ni wa kwake ingawa Gigy kwa ajili ya hasira
anampa mtoto mpenzi wake wa sasa.
Baada
ya povu hilo Gigy Money ameibuka na kuomba radhi kwa maneno aliyoongea
huku akidai ilikuwa ni hasira ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram
ameweka ujumbe huu:
No comments