Aliyechora katuni ya netanyahu afukuzwa kazi
Mchoraji katuni maarufu wa Ujerumani amefukuzwa kazi baada ya kuchora picha ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Katuni hiyo iliyochorwa na Dieter Hanitzsch imemuonyesha Netanyahu akiwa amebeba kombora katika mkono wake mmoja.
Ameonekana amevaa nguo kama mwanamuziki maarufu wa Israel Netta Barzilai aliyeshinda katika amshindano ya Eurovision.
Picha hiyo imeambatana na maneno,"Mwaka kesho Jerusalem."
Mhariri mkuu wa gazeti hilo Wolfgang Krach ameomba radhi huku mchoraji mwenyewe akikataa kufanya hivyo.
Dieter Hanitzsch amekataa kuomba radhi na kusema kuwa amechora katuni hiyo maksudi kuuonyesha umaa jinsi Netanyahu alivyoitumia Eurovision kwa manufaa yake mwenyewe.
Vilevile mchoraji huyo mkongwe kabisa mwenye miaka 85 ameshangazwa na gazeti hilo kumfukuza kazi kwani amedai kuwa mara nyingi jambo kama hilo likitokea,mchoraji huonywa lakini sio kufukuzwa.
No comments