Breaking News

Urusi Yazidi Kuionya Marekani......Yasema Shambulio Lolote la Marekani Syria litazua vita vikali dhidi Yao

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, ameonya kuwa shambulio lolote la anga litakalofanywa na Marekani nchini Syria litasabaisha kulipuka kwa vita baina ya Moscow na Washington na kuongeza kuwa Urusi haiwezi kuepuka uwezekano wowote wa kutokea vita baina ya mataifa hayo.

Nebenzia ameituhumu Marekani na washirika wake kwa kuiweka amani ya mataifa katika hali hatari zaidi kwa kile alichokiita sera za ukatili na kusema kuwa hali ilivyo kwasasa ni hatari kupita kiasi.

Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa mataifa ya Ufaransa na Uingereza kujadili juu ya kutoa kauli ya pamoja kwa kile wanachoamini kuwa matumizi ya sialaha za kemikali yaliyofanywa na Syria kwenye maeneo ya kitalii yanayoshikiliwa na waasi.

Hata hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imesema baraza la mawaziri limekubaliana kwamba matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria haipaswi kwenda kinyume lakini hakutoa maelezo ya hatua yoyote inayoweza kuchukuliwa.

Baada ya mkutano wa dharula uliochukua saa mbili mjini London, taarifa isiyorasmi inasema kwamba Theresa May ataendelea kushirikiana kikazi na nchi za Marekani na Ufaransa ili kuratibu mwitikio wa kimataifa.

Wabunge kutoka Chama cha upinzani cha Labour pamoja na Chama cha Usimamizi wa kihafidhina wametaka kura ya turufu ipigwe bungeni kabla ya majeshi ya Uingereza kuchukua dhamana.

No comments