Breaking News

PHILIPPE COUTINHO:MAMBO YAMUENDEA KOMBO BARCELONA

“Philippe Coutinho bado hajafikia matarajio katika kikosi cha Barcelona , kwa mujibu wa mchambuzi wa soka wa Hispania kupitia kituo cha Sky Sports , Terry Gibson.

Coutinho alihamia Barcelona mwezi Januari kutoka Liverpool kwa thamani ya Pauni Milioni 146, akifunga magoli 3 na kutengeneza mawili katika mechi 13 mpaka sasa .

Baada ya kuchelewa kucheza mechi yake ya kwanza kutokana na kuumia misuli ya nyuma ya paja , Coutinho ameonyesha kiasi tu ubora wa kipaji chake na Gibson alikuwa anategemea zaidi.

” Inabidi nikiri , nilikuwa nategemea zaidi kutoka kwa Coutinho , kusema ukweli. Najua kwamba kuna muda wa kuzoea anahitaji, lakini amekuja akiwa mchezaji aliyekamilika, huku Ousmane Dembele ni mchezaji mdogo akiwa amecheza mechi chache sana katika maisha yake ya soka mpaka sasa . Coutinho amekuja akiwa amekamilika.”

Barcelona walifunga mara mbili katika dikaka za majeruhi kwenye mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya Sevilla na kuimarisha rekodi yao ya kutopoteza mechi ndani ya La Liga, lakini Gibson hakuridhishwa na mchango wa Coutinho pindi Barcelona walipouhitaji zaidi.

” Nilipomuangalia wikiendi , ilikuwa wazi kabisa ni tofauti kubwa ilikuwa pindi Lionel Messi alipoingia ndani ya Barcelona.Najua sio haki kuhoji mchango wa Coutinho dhidi ya Messi , lakini hakuchangia pale alipohitajika.’

” Pindi dakika zilivyozidi kusogea mbele alikuwa yupo tayari kupiga pasi rahisi tu , muda ambao ilikuwa ikihitajika zaidi , ilikuwa ikihitajika kwake kuwashambulia mabeki, kupiga mashuti golini na kutengeneza nafasi.”

” Lakini alikuwa anafanya kinyume chake, alikuwa anapata mpira halafu anaachia pasi rahisi na kuna muda hadi anapokonywa mpira.”

Licha ya kutambua kwamba Coutinho amekuwa na nyakati zake nzuri , Gibson amesisitiza kwamba ada kubwa iliyotumika bado haijafanana na kiwango chake mpaka sasa .

” Lazima tuwe na matarajio makubwa kwa Coutinho. Hatutakiwa kuruhusu huu muda wa kuzoea kuweka wingu kwenye hoja zetu hasa akiwa amegharimu kiasi kikubwa.”

” Amekuwa na nyakati zake, amefunga magoli mazuri , ametengeneza magoli mazuri. Ilikuwa mechi ngumu, lakini nafikiri kwamba angeweza kufanya vizuri zaidi.”

No comments