Breaking News

MASHABIKI WA SIMBA KATIKA PRESHA YA UBINGWA,NA MASHABIKI WA YANGA KAWAIDA KWAO

SIMBA KATIKA PRESHA YA UBINGWA,YANGA KAWAIDA KWAO

Hadi kufika mei 26 mwishoni mwa msimu huu ligi kuu ya soka Tanzania bara itakuwa imefika ukingoni,kwa baadhi ya timu hususani mashabiki wengine wakiwa na furaha wengine wakiwa na huzuni yote haya ni kutupa maana halisi ya msemo wa ULICHOKIPANDA NDICHO UTAKACHO VUNA

Kwa sasa ligi kuu hakuna timu iliyokamilika kila idara au hakuna timu yenye uwekezaji mzuri kama simba sc iliyoongezwa utamu na mshinda zabuni MOHEMMED DEWJI ” MO” huo ndio ukweli na utabaki kuwa hivo simba ikikosa UBINGWA msimu huu itakuwa ni ajabu sana na pia itakuwa ni jambo la kushangaza kwa aina ya wachezaji walionao,Desturi ya simba huwa wananza ligi vizuri ila mwisho ni ndio wanashindwa kumaliza wanacheka mwanzoni mwishoni wanalia wakati anayelia mwanzoni mwishoni akicheka ndio mvunaji mzuri,Haitakuwa jambo la ajabu kwa yanga kukosa UBINGWA msimu huu kulingana na aina ya wachezaji iliyonayo kiuwezo wa mchezaj mmoja mmoja wa simba na yanga ukweli ni kwamba simba ina wachezaji wazuri sana,ukiangalia ukata unaowasibu yanga na kuwa na majeruhi waliokaa nje kwa muda mrefu ( Tambwe,Ngoja,Kamusoko) ni jambo ambalo kwa simba lilikuwa ahueni na sasa baada ya kupona simba hatakiwi kupoteza kitu akianza na mechi ya Leo dhidi ya njombe mji.

Kwa sasa ligi ilipofikia ndio pagumu kulingananja aina ya point walizokuwa nazo vigogo hawa wawili wasoka,Ugumu unachagizwa na aina ya matokeo waliyoyapata katika mashindano ya AZAM SPORTS FEDERATION CUP (FA),Vigogo hawa wawili wameaga mashindano hayo na vita imehamia VPL.Mechi itakayowakutanisha watani hawa ndio itakayoanza kutoa taswira ya nani atakuwa bingwa kwa msimu huu,Simba ndio wako katika presha ya ubingwa kuliko yanga na presha ni kutokana na desturi ya simba kuanza vizuri na kumaliza vibaya,na yanga kuanza vibaya na kuja kunyang’anya tonge mdomoni.

Kitu kikubwa cha simba ni kutokuruhusu makosa ya makosa ya misimu iliyopita,wanahitaji kushikamana zaidi ili waweze kutwaa ubingwa ambao kwao utakuwa ni furaha sana kwa kombe hilo walilolikosa kwa miaka mitano,Kwa fikra zangu haitakuwa ajabu kwa yanga kukosa ubingwa kutokana na namna matatizo yanayowakabiri kuliko simba kiuwekezaji na uwezo wa mchezaj mmoja mmoja ni wazuri kuliko Yanga

Credit Said mwalimu

No comments