Mambo 10 Unayotakiwa Kufahamu Kutoka kwa Wanawake

1. Tamaa zao. 

Mwanamke yeyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa Mama yako.

2. Hulka zao.

Wanawake wote huonesha upendo wao waziwazi isipokuwa wale waliotendwa kabla.

3. Kuachana.

Mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha kula swala, Mwanamke kumuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia Simba mzee.

4. Tabia.

Jihadhari na maneno ya vijiweni kwamba wanawake wote wako sawa kitabia. No, lakini kumbuka hakuna Mwanamke asie Mwanamke.

5. Mpenzi wa zamani.

Kujaribu kumsahau mwanamke uliyewahi kumpenda ni kama kumkumbuka mtu usiyemjua. Ni ngumu.

6. Kuoa.

Muhimu kuoa, na ni ngumu sana Kumjua mke mwema kabla ya kuoa, ni waigizaji wazuri sana. Kumbuka maneno ya Albert. " Muhimu kuoa, ukipata mke mwema utakuwa na furaha, ukipata mke mwovu utakuwa mwanafalsafa.

7. Usaliti.

Vizuri kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa, la usipojiandaa ama waweza kuua mtu au hata kujiua. ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe, hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyokuwa hai.

8. Pesa na Mapenzi.

Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni, hapa duniani ni ngumu mno, lakini usihofu sana, kuna makubaliano bila pesa. Omba Mungu.

9. Uongo.

Wahenga walisema Ukweli unauma, Na mimi nakuambia "Uongo unaua"

10. Kumjua wanamke yahitaji muda wa kmchunguza sana.

Kutaka kumjua mwanamke unahitaji miaka mingi ya kuishi kuliko idadi ya nywele zao. Soma vitabu, makala, majarida, filamu, nyimbo na hotuba za wanaofundisha mandhari za wanawake. Kuna kanuni moja tu ya kupenda, " ili ubaki salama katika kupenda sharti ujipende kwanza".

No comments