Kikosi cha Simba Kipo Tayari kwa Kufa na Kupona Dhidi ya Mbeya City
Kikosi cha klabu ya Simba kimeanza rasmi mazoezi yake hii leo kwenye uwanja wa Boko Veteran jijiini Dar es Salaam kujiandaa kuwakabili Mbeya City.
Simba SC imeanza mazoezi hayo kwaajili ya kujiwinda na mchezo wao dhidi ya Mbeya City utakao pigwa tarehe 12.04.2018.
Simba inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 52 dhidi ya 46 za Yanga SC anaeshika nafasi ya pili.
Klabu hiyo ya soka yenye maskani yake mitaa ya k/koo inapamba kufa na kupona ili kujihakikishia inafanikiwa kutwaa taji la ligi kuu soka Tanzania Bara ambalo wamelikosa kwa miaka mitano sasa huku likiwa linatetewa na mahasimu wao Yanga SC waliyochukua mara tatu mfululizo.
No comments