MATATIZO YA MAWE KWENYE FIGO NA TIBA YAKE
UGONJWA wa mawe kwenye figo siyo mgeni miongoni mwa watu hivi sasa, hasa wenye umri mkubwa. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaamu linajulikana kama ‘Gallstones’.
Mawe ya kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo na wakati mwingine huwa vikubwa mfano wa dole gumba. Hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.
Tiba ya tatizo la mawe kwenye figo, mara nyingi huwa ni upasuaji wa kuvitoa na hugharimu fedha nyingi na pia husababisha maumivu wakati wa kufanya oparesheni hiyo. Lakini kwa kutumia tiba mbadala ya vyakula, unaweza kuondoa mawe hayo bila kufanya oparesheni.
Maelezo haya huwezi kuambiwa na daktari hospitali hata siku moja lakini kwa kusoma makala kama haya utajifunza njia nyingine ya kuutibu mwili wako kwa njia ya vyakula. Kama mawe yaliingia tumboni kwa njia ya vyakula, bila shaka yanaweza kutoka pia kwa vyakula.
JINSI YA KUONDOA MAWE KWENYE FIGO
Kuna tiba mbadala za aina nyingi, lakini katika makala yangu ya leo nitawajulisha njia mbili unazoweza kuchagua moja wapo. Moja ni kufanya kwa muda wa siku sita mfululizo na nyingine ni ya kufanya kwa siku moja tu, chaguo ni lako.
NJIA YA SIKU SITA
Katika siku tano za kwanza, kunywa juisi halisi ya Tufaha(pure apple juice) glasi kubwa nne kila siku kwa siku tano mfululizo. Au kula tufaha nzuri tano badala ya juisi. Ili kuwa na uhakika na juisi halisi, ni vyema ukanunua tufaha za kijani (green apple) na ukatengeneza juisi mwenywe. Juisi hii au matufaha hayo yatafanya kazi ya kulainisha kwanza mawe tumboni.
Siku ya sita, anza siku yako kwa kula mlo wako wa kawaida hadi saa nane mchana, kuanzia saa nane utatakiwa ufunge usile kitu chochote mpaka asubuhi siku inayofuata ndiyo ule chakula chako.
Ifikapo saa 12 jioni, kunywa kikombe au glasi moja kubwa ya maji uliyochanganya na kijiko kimoja kidogo cha ‘Magnesium Sulphate’ . Weka maji kwenye glasi au kikombe, chukua ‘Magnesium Sulphate’, chota kijiko kimoja kidogo, tia kwenye maji hayo na changanya, kisha unywe mara moja. ‘Magnesium’ husaidia kufungua njia.
Ifikapo saa mbili usiku, rudia kunywa mchanganyiko huo wa maji na ‘Magnesium’. Baadaye saa 4 usiku, changanya nusu kikombe cha juisi halisi ya limau (fresh lemon juice) na nusu kikombe cha mafuta halisi ya mzaituni (pure olive Oil). Hiki ndiyo kitakuwa kinywaji chako cha mwisho kwa usiku huo, kisha nenda kalale.
Vinywaji hivyo vitasaidia mawe kutoka kwa njia ya haja kubwa bila shida. Usiku huo huo, unaweza kusikia haja ya kwenda chooni, au vinginevyo utasikia asubuhi.
NJIA YA SIKU MOJA
Ukisha kula chakula chako cha usiku, usile kitu kingine tena hadi kesho yake asubuhi ambapo utakunywa glasi kubwa tatu za juisi ya tufaha za kijani. Usile kitu kingine hadi mchana unywe tena juisi ya tufaha 3. Usile kitu kingine tena hadi usiku wakati wa chakula cha usiku, unywe tena juisi ya tufaha kubwa 3 za kijani kama mlo wako wa usiku.
Iwapo utashindwa kutengeneza juisi mwenywe, basi bora ule tufaha zenyewe kiasi kilichotajwa. Katikati ya mlo na mlo, utaruhusiwa kunywa maji ya kawaida tu na siyo kitu kingine. Hii ina maana utafunga siku moja kwa kula tufaha na maji tu.
Muda mfupi kabla ya kwenda kitandani, tengeneza juisi halisi ya malimau matatu, changanya na nusu kikombe cha mafuta ya mzaituni (Pure olive oil) kunywa kisha panda kitandani, kinywaji kinaweza kisiwe na ladha nzuri, lakini usijali, ndiyo dawa.
Ukiwa kitandani, lalia ubavu wako wa kulia na ukunje magoti kadiri uwezavyo na ulale hivyo kwa muda utakaoweza au hadi hapo utakapopitiwa na usingizi. Ulalaji wa aina hii huwezesha utokaji wa mawe kwenye figo na kwenda tumboni kwa ajili ya kutoka kwa njia ya haja kubwa.
Ukijisikia haja ya kwenda chooni, fanya hivyo haraka, vinginevyo utalala hadi asubuhi ndiyo utakwenda chooni. Ili kuona kama vimawe vimetoka, weka utaratibu wa kukagua haja yako na utaona vitu rangi ya kijivu au kijani vinavyong’aa na hapo utakuwa umefanikiwa.
No comments