Breaking News

REAL MADRID IMETENGA £53M KWA AJILI YA SERGIO AGUERO WA MANCHESTER CITY

Real Madrid wameonyesha nia yao kumsajili straika wa Manchester City Sergio Aguero, kwa mujibu wa habari

Mshambuliaji huyo wa Argentina amekuwa katika kiwango safi kwa vinara wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu, akifunga magoli 10 katika michuano yote.

Real, kwa upande mwingine, wameripotiwa kujiandaa na maisha bila ya Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema, ambao tetesi zimevuma kuwa wote wanatafuta mlango wa kutokea Bernabeu.

Kwa mujibu wa Don Balon, rais wa Blancos Florentino Perez amekuwa akivutiwa kwa muda mrefu na Aguero mwenye umri wa miaka 29 na anaandaa kitita cha £53m kumleta mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid La Liga.

Hata hivyo, habari zimedai kuwa kufanikiwa kwa dili hilo kutategemeana na uwezo wa Man City kumpata Alexis Sanchez kwa uhamisho huru kutoka Arsenal mwisho wa msimu.

Aguero amefunga mara 179 na kutoa pasi 54 za goli kwa City tangu atue Etihad akitokea Atletico 2011.

No comments