LWANDAMINA AZIPANIA POINTI TATU ZA SINGIDA UNITED
Kikosi cha Yanga kitakuwa cha kwanza kuutumia uwanja wa Namfua, wakati Jumamosi kitakapo cheza na wenyeji wao Singida United
Kocha ya Yanga George Lwandamina, amesema pamoja na kikosi chake kuwakosa nyota wanne wa kikosi cha kwanza katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Singida United, lakini anauhakika wa kuibuka na ushindi.
Lwandamina ameiambia Goal, kuwakosa Juma Abduli, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko na Amissi Tambwe, kinamuumiza akili lakini chipukizi waliopo kwenye kikosi hicho wanampa jeuri na kuamini aanaweza kushinda mchezo huo.
“Inaumiza kuwakosa wachezaji wako wakutegemea kwenye mchezo muhimu kama huo, lakini kinachonipa faraja nikwamba wachezaji hao hawana msimu mzuri tangu mwanzo wa msimu na vijana waliopo wamekuwa wakitekeleza vyema majukumu ya timu ndiyo maana leo Yanga, ni miongoni mwa timu mbili zilizopo kwenye nafasi za juu,” amesema Lwandamina.
Mzambia huyo amesema anachokifanya hivi sasa ni kujenga timu ambayo haitamtegemea mchezaji mmoja, na hilo limeanza kujionyesha kwani tangu kuanza kwa msimu huu nyota hao hawana mchango mkubwa kwenye kikosi chake kutokana na kukabiliwa na majeruhi.
Lwandamina amesema anaheshimu uwezo wa wachezaji hao na mchango wao ni mkubwa lakini, kwa kipindi hiki walichokuwa majeruhi ataendelea kuwatumia vijana hao huku akisubiri waweze kupona na kurejea kumuongezea nguvu kwenye mechi zilizosalia za mzunguko wa kwanza.
Yanga inatarajia kuondoka Dar es Salaam, leo wakielekea mkoani Singida, ambapo Jumamosi wataikabili Singida United kwenye pambano, ambalo litapigwa uwanja wa Namfua mkoani humo.
No comments