Breaking News

JESHI LA ZIMBABWE: TUNAWALENGA WAHALIFU SIO MUGABE


Jeshi la Zimbabwe limesoma taarifakwenye kituo cha runinga cha serikaliZBClikisema kuwa linachukua hatua yakuwalenga wahalifu.
Hata hivyo limesema kuwa hayo siomapinduzi ya kijeshi na Rais Mugabeyuko salama.
Milio mikubwa ya risasi ilisikika katikamaeneo ya kaskazini mwa mji mkuuHarare mapema leo.
Taarifa hiyo ya jeshi ilikuja saa kadhaabaada ya jeshi kudhibiti kituo cha ZBC.
Mwanamume mmoja ambaye alikuwaamevaa sare za jeshi alisema kuwajeshi linataka kukabiliana na watuambao wanatenda uhalifu unaoletamadhara ya kijamii na kiuchumi nchiniZimbabwe.
"Wakati tutakapomalzia wajibu wetu,tunatarajia kuwa hali itadudi kuwasawa."
Taarifa hiyo ilisema kuwa Mugabe 93,na familia yake wako salama.
Image caption
Wanajeshi wakiwa na silaha nzitowameoneakana wakirandaranda mjiniHarare
Haijulikani ni nani anaongoza hatua hiyoya kijeshi.
Magari ya wanajeshi waliojihami kwasilaha yameonekana maeneo ya mjiniHarare.
Hali hiyo ya wasi wasi wa lolote kuwezakutokeaimeanza hapo jana jioni,ambapo wanajeshi wakiwa na silahawalionekana wakijipanga katika maeneokadhaa pamoja na kuzingira ofisi zashirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC.
Rais Robert Mugabe amemfuta kaziMakamu wa Rais
Hata hivyo taarifa zinasema kuwawafanyakazi wa shirika hilo lautangazaji ZBCwaliambiwa nawanajeshi hao kwamba hawapaswikuwa na wasiwasi na kwamba uwepowa vikosi hivyo ni kwa lengo la kulindaeneo hilo.
Milipuko mizito imeendelea kusikikapia.
Image caption
Mkuu wa jeshi la Zimbabwe ConstantinoChiwenga alitahadharisha uwezekanowa jeshi kuchukua nchi
Chama tawala nchini Zimbabwe kimemtuhumu mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga, kwa hatua yake ya madai kuwa jeshi lipo tayari kuingilia mzozo huo wa kisiasa kwa lengo la kulinda wapigania uhuru wa taifa hilo.
Bi Grace Mugabe ataka makamu wa rais afutwe kazi
Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Rais Robert Mugabe kutokana na hali ya sasa nchini mwake.
Marekani imesema kuwa inafuatilia kwa karibu hali ya Zimbabwe na kutoa rai pande zote kutatua mzozo huo kwa njia ya amani.
Image caption
Grace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe
Naye Balozi wa Marekani nchini Zimbabwe kupitia ukurasa wake wa Tiwtter amesema kuwa leo watasitisha shughuli za kiofisi ubalozini hapo kutokana na halisi ya sasa mjini Harare.
Balozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini Isack Moyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa serikali ipo imara katika jambo hilo na kuzuia uwezekano wowote wa kufanyika kwa mapinduzi.

No comments