Breaking News

Watu 50 wafariki katika shambulio la muziki Las Vegas

Tamasha la muziki la Route91 Harvest Festival, limeingia dosari  kutokana na mitutu ya bunduki ilikuwa ikipigwa kuelekezwa katika tamasha hilo ambapo watu 50 wamefariki kutokana na shambulio hilo huku wengine 100 ni majeruhi.

Shambulio hilo limetokea wakati msanii Jason Aldean, akiwa anakamilisha ratiba ya kutumbuiza usiku wa tamasha hilo ghafla kukasikika milio ya risasi ikitokea katika ghorofala 32 kwenye hotel ya Mandalay Bay Resort and Casino ambapo mtu mwenye bunduki Stephen Paddock(64) alikuwa akifatua risasi hizo.

Kikosi cha usalama cha Marekani walifanikiwa kufika katika hoteli hiyo na kumtia nguvuni muhusikia  huyo ila bado wakazi wa maeneo hayo wanahofu kuwa bado kuna kundi kubwa waliotekeleza shambulio hilo ila sio mtu mmoja.

 

No comments