Breaking News

WAFUASI WA UPINZANI KENYA WAANDAMANA KUSHINIKIZA MAGEUZI IEBC


Polisi walirusha gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji kadha waliokusanyika NairobiHaki miliki ya pichamasangula blog
Image captionPolisi walirusha gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji kadha waliokusanyika Nairobi
Wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) wamejitokeza katika baadhi ya miji nchini humo kushinikiza kuondolewa kazini kwa baadhi ya maafisa wakuu wa tume ya taifa ya uchaguzi.
Maafisa wa usalama Kenya wamekuwa kishika doria karibu na jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) jijini Nairobi.
Muungano wa Nasa ukiongozwa na Raila Odinga umetangaza maandamano ya kila Jumatatu na Ijumaa kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Hayo yakijiri, mabalozi kutoka nchi kadha za Magharibi wameilaumu serikali ya Kenya pamoja na upinzani, kabla ya kufanyika kwa shughuli za upigaji kura baadaye mwezi huu.
Kwa njia ya taarifa ya pamoja wanadiplomasia wa mataifa 13 na jumuia ya bara Ulaya EU, walikosoa upinzani nchini Kenya kwa kutishia kususia marudio ya uchaguzi mkuu, na chama tawala kwa kujaribu kubadilisha sheria za uchaguzi katiba kabla ya marudio ya uchaguzi huo mkuu.
PolisiHaki miliki ya pichaREUTERS
Maandamano NairobiHaki miliki ya pichaREUTERS
Mfuasi wa upinzani akiwa amebeba bango Nairobi
Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba lakini Nasa wanasema sharti mabadiliko yafanywe kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika uchaguzi huo.
Polisi akishika doria

No comments