Breaking News

Samatta kuiongoza Genk

Mehi hiyo ya Ligi Kuu inatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na rekodi ya timu hizo ambazo katika mechi za hivi karibuni zimekutana mara 17 na Genk kupoteza 10.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye wiki iliyopita alipika bao la kusawazisha ambalo liliifanya timu yake isipoteze nyumbani, anategemewa kuiongoza Genk kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu Ubelgiji keshokutwa Jumapili dhidi ya Anderlecht.

Rekodi zinaonyesha kwenye michezo 17 ya hivi karibuni kwenye mashindano yote ambayo timu hizo zimekutana, Genk ya Samatta imekuwa ikipata wakati mgumu kupata ushindi.

Genk imepoteza michezo 10 mbele ya Anderlecht, suluhu mara 3 na kushinda mara 4 pekee hata hivyo ndani ya michezo hiyo zimetoka kadi nyekundu mara 8 hivyo ni mchezo ambao utakuwa na ushindania wa aina yake.

No comments