Breaking News

NAZI ZILIZOANDIKWA KIARABU UWANJANI ZAZUA GUMZO LIGI KUU

a zinashika kasi katika soka la Tanzania, matukio yanayohusisha imani hizo yamekuwa yakiendelea kutokea kwenye viwanja tofauti, kabla, wakati wa mchezo na hata baada.

Ligi Kuu ya Zanzibar imeshaanza upande wa Unguja na tayari baadhi ya mambo yameonekana kutawala kuhusu imani hiyo.

Ndani ya Uwanja wa Amaan ambao unatumika kwa ajili ya michezo ya ligi hiyo, juzi kulionekana nazi zikiwa zimevunjwa huku zikiwa na maandishi yanayodhaniwa kuwa ni ya Kiarabu.

Nazi hizo zilikutwa pembeni ya uwanja huo lakini hakukuwa na mtu aliyetoa maelekezo zaidi ya nani alikuwa mhusika au ilikuwaje hadi nazi hizo zikawa eneo hilo

No comments