Breaking News

Morata awabadilikia mashabiki wa Chelsea


Asisitiza kwamba hata Chelsea ikimuongezea miaka 10 yupo tayari kuendelea kubaki London.

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata amewatoa hofu mashabiki na uongozi wa klabu hiyo kwamba ataendelea kuitumikia klabu hiyo hata baada ya mkataba wake kumalizika.

Morata amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kueleza kwenye mahojiano na Gazeti la Dello Sport kuhusu kuondoka England baada ya mkataba wake kumalizika.

Alisisitiza kwamba nia yake ni kuitumikia Chelsea kwa miaka 10 baadaye, jambo ambalo limeondoa hofu kwa mashabiki  kwamba mchezaji huyo angetimka London baada ya mkataba wake kumalizikika.

Pia alisisitiza kwamba anafurahia maisha ya kucheza soka Stamford Bridge ambako amesajiliwa kuihudumia timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano alipowasili Juni mwaka huu akitokea Real Madrid.

Aliongeza kuwa Jambo la msingi kwake ni kuwa katika kiwango kizuri wakati wote na kuimarika zaidi.


No comments