Breaking News

INASEMEKANA MAYANJA AMEACHANA NA SIMBA ILI AENDE KAGERA SUGAR



Kocha msaidizi wa Klabu Ya Simba,Jackson Mayanja jana ameachana na kalabu hiyo kwa kile alichokisema ni sababu za kifamilia.

Taarifa za siri kutoka kwenye vyanzo vyetu vya kuaminika zinasema,Kocha mayanja anahitajika na Kagera Sugar kuwa kocha mkuu  kuchukua mikoba ya Meck Maxime.

Maxime anaondolewa kwenye klabu hiyo kutokana na kuanza vibaya kwa msimu huu ambapo imepelekea klabu hiyo kushika mkia kwenye msimamo wa ligi.

Inasemekana uongozi wa Kagera sugar umemuahidi donge nono kocha mayanja ili arejee kwenye klabu hiyo ambayo ni klabu yake ya kwanza kuifundisha hapa Tanzania

No comments