Breaking News

“Habari ya kuondoka kwa Mayanja imekuuzwa lakini ameondoka Mwambusi Nchi Yote Kimya"- Haji Manara

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba, Haji Manara amesema Simba SC ilimuomba kocha, Jackson Mayanja iwavumilie mpaka itakapomalizana na Irambona Juma .

Manara ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari alipokuwa akimtambulisha mrithi wa kocha Mayanja na meneja mpya, Richard Robert.

“Hatukupanga mwalimu Mayanja aondoke ila alikuwa na matatizo na familia yake ambayo na alituomba ruksa kwa muda mrefu ila Simba SC tulimuomba  atuvumilie mpaka tutakapo maliza mazungumzo na kocha mwingine.”Amesema Manara.

Manara ameongeza “Bahati nzuri tumempata kocha bora wa mwaka jana wa Rwanda akiwa bingwa wa klabu ya Rayon lakini stori ya kuondoka kwa Mayanja imekuwa habari kubwa.

“Habari ya kuondoka kwa Mayanja imekuuzwa lakini ameondoka M wambusi‘no bady talk, this is Simba’ yani ndo hapo muone ‘brand’ ya Simba ilivyokubwa mtakataa, mtabisha maana alivyoondoka hakuna mtu aliyesema nchi imekaa kimya kaja kocha huyu watu wanazungumzia Masoud Juma ndiyomaana nasema hii ndiyo Super Brand ya nchi.”

Klabu ya Simba imeamua kuachana na kocha wake raia wa Uganda, Jackson Mayanja hapo juzi siku ya Jumatano hali iliyozua minong’ono miongoni mwa wapenzi wa mchezo wa soka nchini kwakuonekana swala hilo kama limekuja ghafla.

Irambona Juma alikuwa alichaguliwa kuwa kocha bora nchini Burundi kupitia klabu ya Rayon Sports hivyo wacha apewe muda na kusubiri hekima na demokrasia za wakati kuweza kutoa matokeo ambayo yamefichwa nyuma ya msare wa saa

No comments