Breaking News

WAZIRI MWIJAGE ALIA NA MATAPELI

Matapeli wanaofanya shughuli za udalali wa kitapeli wa zao la korosho nje ya nchi wachafua jina la Tanzania nchini India. 

Hayo yamesemwa leo Jumatatu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa habari. 

Amesema anaoushahidi unaotosheleza kuwafikisha mbele ya sheria kampuni hizo za kidalali nje ya nchi. 

“Vitendo hivi vinavyofanywa na makampuni haya havivumiliki kwani mchezo huu ni mauti kwetu na nitahakikisha wanachukuliwa hatua kwani ninao ushahidi  unaotosheleza,”alisema Mwijage. 

Alisema watu wametapeliwa kwa kuambiwa pindi wanapoagiza mazao kuwa watoe pesa ya kianzio ambayo ni kuanzia dola za Marekani  123,000,  sawa na Sh275 milioni na dola 200,000 sawa na Sh448milioni za kitanzania. 

“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira  ilisababishwa uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage. 

Mwananchi;

No comments