REFA WA KIKE ATENGENEZA HISTORIA BUNDESLIGA
Historia mpya imeandikwa katika ligi kuu ya Ujerumani – Bundesliga, inawezekana jambo ambalo hapa Tanzania tumelizoea kuona mama/dada zetu wakiongoza michezo ya soka nchini lakini leo nchini Ujerumani, mwanamama Babiana Steinhaus amekuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha mchezo wa Bundesliga.
Babiana Steinhaus alisimamia mchezo wa Bundesliga kati ya Werder Bremen ambao walitoka sare na Hertha Berlin jumapili ya leo.
Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye pia na ofisa wa Polisi wa jeshi la Ujerumani, alijiunga na Bundesliga mnamo mwezi May 2017 baada kutumikia katika ligi daraja la pili kwa miaka 6.
Babiana alisimamia mchezo wa Bayern dhidi ya Chemnitzer mnamo August, pia alisimamia mchezo wa fainali ya Champions League ya wanawake, pia alichezesha katika michuano ya Euro 2017.
Hivi karibuni Lorraine Watson alikuwa mwanamama wa kwanza kuchezesha ligi ya wanaume ya Scotland ya Daraja la pili, wakati Edinburgh City walipoifunga Berwick 1-0.
No comments