PAPA FRANCIS KUWASILI COLOMBIA ZIARA YA SIKU TANO
Papa Francis anatarajiwa kuwasili mji mkuu wa Colombia, Bogota saa chache kutoka hivi sasa, ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na Papa nchini humo ndani ya miongo mitatu.
Katika ziara yake ya siku tano, anatarajiwa kugusia mazungumzo ya amani yaliyofikiwa mwaka jana kati ya serikali na kikosi cha waasi cha Farc.
Kuelekea ziara hiyo, waasi wa ELN ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo, wamekubali kuweka silaha chini kwa muda na kufanya mazungumzo ya amani,tukio ambali Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ameliita ni miujiza kabla ya ujio wa Papa.
No comments