OKWI ATOBOA SIRI
Baada ya kutupia mabao mawili dhidi ya Wadui FC kwenye mchezo ambao Simba imeichabanga Mwadui goli 3-0, Emmanuel Okwi amesema juhudi, ushirikiano na wenzake ndiyo siri ya mafanikio yake.
Emmanuel Okwi
Okwi amesema ushirikiano wake na wenzake ndiyo umemfanya kufikisha mabao 6 katika mechi tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Ushirikiano na wenzangu ndiyo jambo namba moja zaidi, nimefanikiwa kufunga mabao mawili na kufikisha sita kwa kuwa tunashirikiana na wenzangu, nawashukuru, Kingine ni juhudi lakini pia kumuamini Mungu kutokana na ninachokitaka,” amesema Okwi kwenye mahojiano yake na vyombo vya habari baada ya kumalizika kwa pambano hilo.
Katika mechi ya kwanza ambayo Simba ilishinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting ambayo ilikuwa ya ufunguzi wa ligi, Okwi alifunga mabao manne, na mpaka sasa ndiye kinara wa kutupia magoli mengi kwenye VPL akiwa na idadi ya magoli 6.
No comments