Mfanyabiashara auawa kwa kupigwa risasi
Polisi imesema inawashikilia watu wanne kwa mahojiano kuhusu mauaji ya mfanyabiashara huyo.
Mfanyabiashara wa Lupa Tingatinga wilayani Chunya, Nestory Kyando ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliovamia nyumbani na dukani kwake.
Katika tukio hilo lililotokea saa tatu usiku wa kuamkia jana Jumapili watu hao walipora Sh4 milioni.
Taarifa zinaeleza mfanyabiashara huyo aliyekuwa akiuza bidhaa kwa jumla alivamiwa nyumbani ambako waliomvamia walimnyang’anya ufunguo wa sefu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema watu wanne wanashikiliwa kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.
Amesema baada ya mfanyabiashara huyo kunyang’anywa ufunguo, watu hao walienda dukani ambako aliwafuta kwa nyuma ndipo alipopigwa risasi.
No comments