Breaking News

KUTANA NA KIJANA WA KISOMALI ALEETENGENEZA SIMU YAKE MWENYEWE


Image captionMo Omer anatarajia kuuza zaidi simu alizotengeneza katika mataifa hasa ya Afrika

Kijana wa miaka 17 kutoka nchini Canada ambaye alijitengenezea mwenyewe simu baada ya mama yake msomali kusema kuwa hana uwezo wa kumnunulia simu ya smartphone amezungumza na BBC.

Mo Omer - ambaye anajiita mwenyewe "tech nerd" - alitengeneza simu ya smartphone kuanzia mwanzo , na anasema ataiuza kwa dola $180 Shilingi 403,726.76 za kitanzania.

"Ina kila kitu unachoweza kukipata katika simu ya kawaida, ni kwamba tu haina gharama kubwa ," ameiambia BBC.

Simu "sio vifaa vigumu kutengeneza", aliongeza- na akasema ana azma ya kuzipeleka katika baadhi ya maeneo ya Afrika.

"Tumepokea maombi kutoka Nigeria na Algeria na maeneo mengine mengi. Ni soko linalokua kwa kasi ambalo tungependa kuingia

No comments