KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA ASIMULIA WALIVYOONYESHWA MIILI YA WATOTO SHIMONI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amefunguka na kusema kuwa jeshi hilo linaendelea kumshikilia kijana Samson Peter (18) ambaye anadaiwa kuwateka watoto wanne na kusababisha vifo vya watoto wawili mkoani Arusha.
Kijana huyo ambaye alikamatwa mkoani Geita akiwa na mtoto mwingine ambaye inasemakana alimteka tena, alipobanwa na jeshi la polisi alikiri wazi kuwa aliwateka yeye hao watoto wanne na kusema kuwa wawili aliwatumbukiza kwenye shimo la choo ambalo lilikuwa halijaanza kutumika kabla ya kwenda Geita ambapo mwisho wa siku walipatwa na umauti.
"Tulipo mbana aliweza kukiri kwamba anahusika na utekaji wa watoto na alisema kuwa tayari ameshawadhulu hivyo tuliongozana naye mpaka Olasiti ambapo aliweza kuonyesha sehemu ambapo alikuwa amewaua hao watoto na kuweza kuwatumbukiza kwenye shimo la maji machafu katika nyumba mbayo ilikuwa imejengwa hivi karibuni na ilikuwa haikaliwi na mtu yoyote" alisema Kamanda Mkumbo
Aidha Mkumbo anasema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na kusema pindi uchunguzi ukikamilika wataweza kumfikisha kijana huyo katika vyombo vya sheria, hata hivyo kamanda Mkumbo anadai jeshi la polisi linachukua hatua mathubuti kuweza kuwapata watu wote waliohusika katika utekaji huo.
"Bahati nzuri watoto wawili waliweza kupatikana mapema hivyo tuliendelea na kuwatafuta watoto wengine wawili pamoja na huyo mtu aliyehusika na utekaji wa watoto hao, watoto ambao hawakuweza kupatikana mapema mmoja alikuwa anaitwa Mauren David Ernest (6) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Lucky Vicent na wa pili Ikram Salum (3) ambaye alikuwa ni mtoto mdogo" alisema Mkumbo
No comments