Breaking News

Hii ndio rekodi ya Real Madrid iliyovunjwa na Real Betis

Usiku wa September 20 2017 club ya Real Madrid ilirudi katika uwanja wake wa Santiago Bernabeu kucheza mchezo wao wa Ligi KuuHispania dhidi ya Real Betis, Madrid walirudi wakiwa na staa wao Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa amefungiwa game nne na LaLiga.

Real Betis wamefanikiwa kuondoka na point tatu Santiago Bernabeu baada ya kuifungaReal Madrid kwa goli 1-0, goli la Real Betislikifungwa dakika ya 90  na Sanabria Ayala, kipigo hicho kinavunja rekodi mbili za Real Madrid ambapo game hiyo ndio inakuwa ya kwanza kumalizika kwa Real Madrid kutofunga goli toka April 2016 dhidi ya ManCity (0-0).

Real Madrid pia wanashindwa kuendeleza rekodi yao ya kupata ushindi katika michezo 73 mfululizo, rekodi ambayo ilidumu kwa miaka baada ya kuwekwa na club yaSantos mwaka 1963, Real Madrid wameifikia rekodi hiyo ya Santos lakini wameshindwa kuivunja.

No comments