SINGIDA KUZIVAA TIMU ZA CONGO
Wachezaji wa timu ya Singida United wakifanya mazoezi.
KATIKA kuhakikisha kuwa timu ya Singida United, inafanya vema katika Ligi Kuu Baramsimu ujao, kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Var der Pluijm, amesema timu yake inatarajia kucheza michezo ya kirafiki nchini Congo na Uganda.
Kocha huyo amesema lengo la kufanya hivyo ni kuijenga timu yake kuelekea Ligi Kuu Bara msimu ujao inayotarajiwa kuanza Agosti 26. Pluijm ambaye mpaka sasa ameiongoza timu yake kucheza michezo miwili ya kirafiki, ambapo mchezo wa kwanza iliichapa Pamba kwa mabao 5-0 na mchezo wa pili akaifunga Alliance kwa bao 2-0, amesema kuwa kadiri siku zinavyokwenda timu yake inaimarika zaidi.
Wakiongea jambo wakati wa mazoezi.
“Nimeiona timu yangu katika michezo miwili ambayo tumecheza, kimsingi naona maendeleo makubwa na tutaendelea kucheza michezo mingi zaidi ili Singida iweze kufanya vyema katika ligi,” alisema. “Mipango iliyopo kwa sasa ni kuhakikisha timu inacheza michezo mingi ya kirafiki na tayari tuko mbioni kwenda Congo na Uganda, kwa ajili ya michezo ya kirafiki,” alisema.
No comments