Rasmi: Alikiba awa mmiliki wa Rockstar
Hit maker wa Aje, Alikiba baada ya kufanya kazi na kampuni ya usimamizi wa kazi zake ya Rockstar4000 kwa takriban miaka 6, Jumatatu hii ametangazwa rasmi kuwa mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Rockstar4000, Muimbaji huyo atakuwa mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo, pia atakuwa Director of Music and Talents.
“Usiku wa jana King Kiba ametangazwa rasmi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television,” ilisema taarifa hiyo.
“Alikiba kwa sasa anakuwa sehemu ya wasanii waliochini ya Rockstar4000 pia anakuwa Director of Music n Talents,”
Rockstar Television inajishughulisha na utengenezaji wa vipindi vya mastara tofauti kutoka nchi mbalimbali na kuvisambaza katika vituo vya Television vya kimataifa.
Kwa sasa nchini Tanzania kampuni hiyo inamsimamia Baraka The Prince, Lady Jay Dee pamoja na yeye mwenyewe.
No comments