Breaking News

MWENYEKITI WA YANGA AFANYA UTEUZI MPYA

Kikao cha utendaji cha klabu ya soka ya Yanga kilichokaa jumamosi ya terehe 15/7  mwaka huu kimeadhimia kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Makao Makuu ya Klabu ya Yanga

Kwa taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo ambao umekaa kikao chake wikiendi hii ni kwamba.

Kwa mujibu wa kikoa cha utendaji kilichokaa tarehe 15/7/2017 na pia kwa mujibu wa katiba ya Yanga Sc idara ya 28:(1)d,Mwenyekiti ana mamlaka ya kujaza nafasi mbili za wajumbe ya kamati ya utendaji zilizokuwa wazi na moja ilioachwa wazi na mjumbe aliekuwa mwenyekiti wa kamati ya mashindano Mhandisi Malume aliekwenda nje ya nchi kwaajili ya masomo.

Wajumbe walioteuliwa na mwenyekiti kujaza nafasi hizo ni,

-Mr.Mohamed Nyenge

-Mr. Tonny Mark

-Mr.Majid Suleiman.

Lakini pia klabu hiyo imefanya maadhimio baada ya kikao cha wachezaji wa zamani na Mwenyekiti.

1.Kuwashirikisha katika masuala ya klabu na kuwaweka karibu na klabu.

2.Kujenga umoja wa wana Yanga kwa ujumla.

3.Kuunda safu ya uongozi wao itakayorahisisha mawasiliano baina yao na uongozi wa klabu.

4.Kuweka kumbu kumbu kwaajili ya historia ya klabu na vizazi vijavyo kupitia wao.

5.Kusaidiana katika suala zima la ugunduzi wa vipaji vya wachezaji kwa manufaa ya klabu.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano

Young Africans Sports Club

17-07-2017.

No comments