Breaking News

Dubai imezindua Magari yasiyotumia dereva yanayoweza kufuatilia wahalifu

Polisi wa Dubai wameanzisha program maalum kutumia magari yasiyokuwa na dereva na yenye kamera maalum kufanya doria kwenye miji mikubwa na sehemu zenye mikusanyiko ili kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa haraka.

Program hiyo itatumia magari hayo yenye uwezo wa kukimbia kwa kasi ya 9.3 mph, kutambua sura za wahalifu wanaotafutwa, kamera aina ya drone inayoweza kumfuatilia mhalifu alipokimbilia na kutambua namba za magari yaliyoibiwa.

Magari hayo yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa inayoweza kunasa matukio yasiyokuwa ya kawaida kutoka umbali wa futi 330 na kutuma taarifa kupitia simu za mkononi kwa Maafisa wa Polisi walio kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu.


No comments